Uchaguzi wa LSK waendelea kote nchini

Dismas Otuke
1 Min Read

Uchaguzi wa chama cha mawakili nchini, LSK umeanza mapema leo Alhamisi kote nchini.

Wanachama wa LSK watawachagua viongozi wa ngazi zote huku kileleta kikiwa kumchagua Rais mpya atakayemrithi Eric Theuri ambaye muda wake wa miaka miwili umemalizika.

Uchaguzi huo unaandaliwa katika mahakama ya sheria kote nchini huku Rais, naibu wake na mwakilishi wa wanaume katika tume ya huduma za mahakama, JSC wakitarajiwa kuchaguliwa.

Shughuli ya upigaji kura inatarajiwa kufungwa saa kumi na moja jioni.

Kiti cha Urais kimewavutia wagombezi watano ambao ni Peter Wanyama, Faith Odhiambo, Bernhard Ng’etich Kipkoech, Harriet Njoki Mboce na Carolyne Kamende.

Kinara anayeondoka Theuri anawania nafafsi katika tume ya JSC akipingwa na Omwanza Ombati.

Share This Article