Uchaguzi Tanzania: Samia Suluhu atangazwa mshindi kwenye Uchaguzi wa Urais

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Samia Suluhu Hassan ametangazwa mshindi mwenye Uchaguzi Mkuu wa Urais wa nchi hiyo.

Tangazo hilo limetolewa leo Jumamosi na mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania INEC, Jacobs Mwambegele.

“Namtangaza Samia Suluhu Hassan kuwa rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,”alisema Jacobs.

Kupitia runinga ya taifa TBC, Mwambegele, alisema Samia aliyewania kupitia tiketi ya chama cha CCM, aliibuka mshindi kwa kupata kura 31,913,866 kati ya 32,678,844 kura zilizopigwa.

Kulingana na mwenyekiti huyo, idadi hiyo inawakikisha asilimia 97.

Uchaguzi Mkuu nchini Tanzania uliandaliwa huku maandamano yakishujudiwa katika miji kadhaa nchini humo, waandamanaji wakitaja ukosefu wa haki.

Website |  + posts
Share This Article