Wakenya hawana sababu ya kuhofu kwani uchaguzi mkuu ujao, utakaoandaliwa Agosti 10, utakuwa wa amani.
Hakikisho hilo limetolewa na serikali kupitia kwa Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen.
Nalo linakuja wakati ambapo visa kadhaa vya kihuni vilivyoshuhudiwa katika mikutano kadhaa ya kisiasa katika siku siku za hivi vikiibua mashaka kuhusu hali itakavyokuwa wakati wa uchaguzi huo.
“Naweza nikatoa hakikisho langu kamili uchaguzi ujao utakuwa wa amani zaidi, isitoshe wenye amani zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Kenya,” amesema Murkomen.
“Tutahakikisha kwamba uchaguzi utakuwa wa amani mno, na kwamba tutakuwa na mazingira mazuri kwa washindani wote kufanya kampeni kwa amani, kupiga kura na matokeo ya nyadhifa mbalibali za uchaguzi kutangazwa katika mazingira ya amani.”
Waziri aliyasema hayo leo Jumatatu alipokutana na Wakuu wa Misheni ya Kundi la Wahisani wa Wakimbizi, wawakilishi kutoka serikali za kaunti za Garissa na Turkana, na maafisa kutoka mashirika ya kimataifa.

Kauli zake zinawadia wakati ambapo mirengo yote ya kisiasa imezidisha kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Nyadhifa zitakazoshindaniwa ni pamoja na urais, ugavana, useneta, ubunge, wadhifa wa mwakilishi wa wanawake na mwakilishi wa wadi.
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC imo mbioni kufanya maandalizi yatakayopisha uchaguzi huo unaotarajiwa kuwa wenye ushindani zaidi katika ngazi zote.