Kenya imejiongezea nishani za dhahabu na fedha huku riadha ikiingia siku ya pili katika michezo ya Olimpiki mjini Dakar,Senegal.
Faith Rono amenyakua dhahabu ya mita 3000 wanawake baada ya kutumia dakika 9 sekunde 15.7.
Yordanos Tsigab wa Ethiopia alishinda fedha huku medali ya shaba ikimwendea Karen Chelimo wa Uganda.

Kenya pia imejiongezea fedha katik fainali ya mita 2,000 kuruka viunzi na maji kupitia kwa Wesley Kipkech kwa muda wa dakika 5 sekunde 36 .28.
June Abdo kutoka Ethiopia amenyakua dhahabu kwa dakika 5 sekunde 29.30, huku Mganda Michael Kibet akiridhia shaba.