Mshambulizi wa zamani wa Nigeria Nwankwo Kanu atawaongoza magwiji wengine wa klabu ya Arsenal kwa mchuano wa kirafiki dhidi ya Harambee Stars Ijumaa hii Novemba 13, katika uwanja wa Nyayo.
Kanu aliye na umri wa miaka 50 ataongoza magwiji wengine wa Arsenal wakiwemo Bacary Sagna, Gervinho, Alex Song, Yaya Sanogo, Tony Adams, Robert Pirès, Ashley Cole, Gilberto Silva, Santi Cazorla, na Theo Walcott.
Victor Wanyama ataongoza kikosi cha magwiji Harambee Stars kinachojumuisha McDonald Mariga, Dennis Oliech, John Bobby Ogolla, Francis Kahata, Francis Onyiso, Jamal Mohammed, JJ Masiga, na Mahmoud Abbas.
Pambano hilo litapigwa uwanjani Nyayo kuanzia saa moja usiku .
Kando na mechi hiyo magjwi hao wa Arsenal wataandaa kliniki ya wakufunzi Jumamosi Novemba 14 katika shule ya Crawford International School.