Ubomozi zaidi watarajiwa kupisha ujenzi wa nyumba za bei nafuu

Dismas Otuke
1 Min Read

Ubomozi zaidi unatarajiwa katika maeneo mbalimbali nchini, huku serikali ikiendelea  kuwafurisha waliovamia ardhi ya umma kupisha ujenzi wa nyumba za bei nafuu.

Waziri wa Ardhi Alice Wahome amefichua kuwa serikali imebaini ardhi ya ekari 12,000 ambayo itajengwa nyumba hizo.

Yamkini baadhi ya ardhi inayolengwa ni ile iliyonyakuliwa na wastawishaji wa kibinafsi, ardhi ya mashirika ya serikali na ardhi ya serikali za kaunti.

Kulingana na Wahome, tayari ubomoaji umeanza katika baadhi ya maeneo kama vile Nairobi, Mombasa, Kisumu na Nakuru.

Serikali inalenga kujenga nyumba zipatazo 200,000 kote nchini.

Share This Article