Uapisho wa Kindiki: Maelfu wamiminika KICC

Dismas Otuke
1 Min Read

Maelfu ya Wakenya, wengine waliosafiri jana usiku hususan kutoka Tharaka Nithi anakotoka Naibu Rais mteule na wakazi wa Nairobi, wamefurika katika ukumbi wa KICC kwa uapisho wa Prof. Kithure Kindiki kuwa Naibu Rais mpya.

Hafla hiyo ambayo itahudhuriwa pia na Rais William Ruto inaendelea katika ukumbi wa KICC huku Prof. Kindiki akiwa Naibu Rais wa kwanza kuteuliwa na Rais na kuidhinishwa na bunge chini ya katiba mpya ya mwaka 2010.

Punde baada ya majaji watatu wa Mahakama Kuu kuruhusu uapisho wa Prof. Kindiki, Katibu wa Baraza la Mawaziri Mercy Wanjau alibuni kamati kuandaa sherehe hizo za uapisho.

Mawaziri, Makatibu wa Wizara, Wabunge, Maseneta, Wakurugenzi wa mashirika ya umma pamoja na mabolozi wa kigeni humu nchini wanahudhuria sherehe hiyo.

Share This Article