Tume ya PSC yajitenga na tangazo bandia la ajira

Tom Mathinji
1 Min Read
Tume ya utumishi wa umma,PSC

Tume ya utumishi wa umma PSC imejitenga na tangazo linalosambazwa kupitia mitandao ya kijamii likidai kuwepo kwa nafasi tofauti za ajira.

PSC imesema matangazo yake yote ya nafasi za ajira yanachapishwa katika magazeti na kwenye tovuti yake. Tume hiyo imesema  imepokea malalamishi ya wakenya ambao tayari wamehadaiwa kwa ahadi ya kazi zisizokuwepo.

“Tume ya utumishi wa umma imejitenga na zoezi la kuwaajiri watu ambalo limetangazwa kupitia mitandao ya kijamii,” ilisema PSC kupitia taarifa.

Tume hiyo aidha imesema haihitaji watu wanaotuma maombi ya kazi kulipa pesa kupitia simu au njia nyingine yoyote ili kuzingatiwa kwa nafasi za kazi zinazotangazwa.

Sasa inatoa wito kwa wanaotafuta kazi za utumishi wa umma kuangalia tovuti sahihi ili kuthibitisha uhalali wa matangazo hayo kabla ya kuchukua hatua nyingine.

Nafasi kadhaa za kazi katika wizara ya madini na uchumi wa bahari, zilikuwa zimetangazwa katika tangazo hilo ghushi ambalo lilishuhudia wakenya wengi wenye matumaini wakituma maombi kufuatia ukosefu mkubwa wa ajira.

TAGGED:
Share This Article