Tume ya kitaifa ya ardhi, NLC kupokonywa mamlaka ya kubaini bei ya ardhi

Dismas Otuke
1 Min Read

Tume ya kitaifa inyosimamia ardhi, NLC itapokonywa mamlaka ya kukagua na kukadiria thamani ya ardhi ya  serikali endapo mswaada unaotazamiwa kuwasilishwa katika bunge la kitaifa na kiongozi wa wengi Kimani Ichung’wah utapitishwa kuwa sheria.

Kulingana na mapendekezo kwenye mswada wa ardhi wa mwaka 2023, Waziri wa Ardhi atapewa mamlaka ya kufanya ukaguzi na kutathimini thamani ya ardhi inayomilikiwa na serikali na yale watu binafsi na wala sio tume ya NLC.

Mabadiliko mengine yanayopendekezwa kwenye mswada huo ni kuwa Waziri atakuwa na uwezo wa kufutilia mbali vibali vya kumiliki ardhi ya serikali vilivyotolewa awali wakati wowote.

Rais William Ruto akiwa katika kaunti ya Isiolo aliwakashifu maafisa wa tume ya NLC kwa kupokea rushwa ili kuweka thamani ya ardhi ya serikali na ya watu kuwa juu au chini na kuahidi kuifanyia marekebisho.

Website |  + posts
Share This Article