Tum azuru kambi ya timu za taifa za wanawake

Dismas Otuke
1 Min Read

Katibu wa Michezo mhandisi Peter Tum alizuru kambi ya timu za taifa za soka za wanawake; Harambee Starlets na wasichana chini ya umri wa miaka 17, katika uwanja wa Kasarani.

Harambee Starlets inajiandaa kukabiliana na Tunisia kesho katika uwanja wa Uinzi Sports Complex kwa mechi ya kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwaka ujao huku wasichana chini ya umri wa miaka 17 wakijiandaa kwa mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia dhidi ya Uganda.

Starlets watazuru Tunisia kwa mechi ya marudio Februari 26 huku mshindi wa jumla akichuana na aidha Nigeria ama Gambia kwa tiketi ya kucheza Kombe la Afrika mwaka ujao nchini Moroco.

Website |  + posts
Share This Article