TSC yaahirisha zoezi la kuwapandisha vyeo walimu kote nchini

Dismas Otuke
1 Min Read

Tume ya Kuwaajiri Walimu, TSC imeahirisha mahojiano ya kitaifa ya kuwapandisha vyeo walimu wa shule za msingi lililoratibiwa kuanza Disemba 4.

Kulingana na taarifa, TSC imelazimika kuahirisha mchakato huo kutokana na mafuriko yanayoshuhudiwa nchini na kutatiza usafiri katika baadhi ya maeneo.

Mahojiano hayo ambayo yangeandaliwa kati ya Disemba 4 na 15 mwaka huu, ni ya kuwapandisha vyeo walimu wa viwango vya C1 hadi C4 katika kaunti zote ndogo nchini.

Kaunti 36 kati 47 nchini zimeathiriwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa inayoyesha katika maeneo mengi nchini.

TAGGED:
Share This Article