TSC, vyama vya walimu mbioni kutibua mgomo wa walimu

Tom Mathinji
1 Min Read
Afisa mkuu mtendaji wa TSC, Nancy Macharia.

Tume ya Kuwaajiri Walimu nchini (TSC) iko mbioni kutibua mgomo wa walimu unaonukia shule zitakapofunguliwa, huku ikiandaa meza ya mazungumzo na vyama vya walimu hapa nchini.

Vyama vya walimu vya KNUT, KUPPET na kile cha wanafunzi wenye mahitaji maalum (KUSNET), vimealikwa kwa mazungumzo hayo leo Jumatano ili kuafikia makubaliano.

Mkutano huo ulioandaliwa na afisa mkuu mtendaji wa TSC, Nancy Macharia ni sehemu ya juhudi za serikali za kujaribu kusuluhisha mzozo wa shiling billion 13.3 wa mishahara ya walimu ambao unatishia kukwamisha masomo katika shule za umma kuanzia wiki ijayo.

Baada ya mkutano huo, vyama vya walimu pia vitakutana kwenye mkutano wa pamoja na maafisa wa Wizara za Leba na Fedha na elimu.

Juhudi za kutafuta suluhisho  zimeongeza kasi kufuatia la agizo la Rais William Ruto kwa Wizara ya Wedha na TSC kutafuta suluhisho kwa mzozo huo wa nyongeza ya mshahara.

Rais WRuto ameziagiza pande zote husika kushauriana na kusuluhisha mzozo huo ili kuepusha mgomo unaonukia wa walimu wa shule za umma.

Website |  + posts
Share This Article