Trump: Marekani haitahudhuria mkutano wa G20 Afrika Kusini

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais wa Marekani Donald Trump.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema taifa hilo halitahudhuria mkutano wa mataifa 20 yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi (G20) utakaoandaliwa Afrika Kusini, kufuatia madai kwamba watu weupe wanadhukumiwa nchini humo.

Kulingana na Trump, ni aibu kwa Afrika Kusini kuandaa mkutano huo ambao unatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa mataifa yaliyostawi zaidi ulimwenguni.

Hata hivyo, wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini, imetaja uamuzi wa Trump kuwa wa kusikitisha.

Hakuna chama cha kisiasa nchini Afrika Kusini kikiwemo kile kinachowawakilisha watu weupe nchini humo kimedai mauaji ya halaiki yanaendelea nchini humo.

Kwenye ukurasa wake wa Truth, Trump alisema,” Ni fedheha kwamba mkutano wa G20 unaandaliwa Afrika Kusini,”.

“Afrikaners (Wazao wa masetla kutoka Ufaransa na Ujerumani) wanauawa na mashamba yao kutwaliwa kinyume cha sheria,” aliandika Trump.

“Hakuna afisa yeyote wa serikali ya Marekani atahudhuria mkutano huo ikiwa ukiukaji wa haki za kibinadamu utaendelea kushuhudiwa,” aliongeza rais huyo.

Awali, Trump alikuwa amesema Afrika Kusini haipaswi kuwa wanachama wa shirika la G20 na kwamba angemtuma makamu wake JD Vance kuhudhuria mkutano huo.

Share This Article