Trump asema hana matatizo ya akili wala uelewa

Martin Mwanje
1 Min Read

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amependekeza kuwa wagombea wote wa uchaguzi wa urais nchini humo wanapaswa kupewa mtihani wa uelewa. 

Matamshi yake yanakuja wakati mpinzani wake Kamala Harris ametilia shaka afya ya akili na uelewa wa Trump wiki chache kabla kuandaliwa kwa uchaguzi wa urais nchini humo.

Uchaguzi huo umepangwa kufanywa Novemba 5 mwaka huu.

“Sina tatizo la uelewa, ila yeye anaweza kuwa nalo,” alisema Trump wakati akiendeleza kampeni zake katika jimbo la Pennsylvania.

“Hakika natoa wito wa watu wote wanaotaka kugombea urais kufanyiwa mtihani wa uelewa. Siyo kulingana na umri,” aliongeza Trump ambaye ana umri wa miaka 78.

Licha ya Harris kutilia shaka afya yake ya akili, Trump amesisitiza kuwa  afya yake ya akili iko shwari na yuko sawa kuingia madarakani.

Share This Article