Trump asema alipigwa risasi kwa ajili ya demokrasia

Marion Bosire
2 Min Read

Aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ambaye pia ni mwaniaji urais wa chama cha Republican amerejelea kampeni baada ya kunusurika jaribio la kumtoa uhai na akaonekana hadharani kwa mara ya kwanza na mwaniaji mwenza JD Vance.

Akizungumza kwenye mkutano wa kisiasa uliohudhuriwa na watu wengi huko Michigan Trump amesema kwamba alipigwa risasi kwa ajili ya demokrasia kwenye jaribio hilo wiki iliyopita.

Trump aliambia wafuasi wake kwamba amekuwa akilaumiwa na chama cha Democrat kwa kuwa tishio kwa demokrasia na sasa yuko tayari kurejea katika ikulu.

Kwa sasa uchunguzi unaendelea kuhusu kisa hicho cha Trump kupigwa risasi kwenye sikio.

Wengi kati ya wafuasi waliojitokeza kwa mkutano wa kisiasa wa Trump katika jimbo la Michigan waliambia wanahabari kwamba tukio la wiki jana halingewazuia kujitokeza kusikiliza mwaniaji wao wa urais.

Mshambulizi alimpiga Trump risasi kwenye sikio na akasababisha kifo cha mfuasi mmoja huku wengine wawili wakiachwa na majeraha ya risasi. Maafisa wa usalama wanasemekana kumuua mshambuliaji huyo papo hapo.

Mkutano wa kampeni wa Trump wa Michigan ambalo ni jimbo linalozozaniwa kisiasa na Republican na Democrat uliandaliwa ndani ya jumba kama mojawapo ya tahadhari za kuzuia tukio la wiki jana.

Huku akishukuru waliohudhuria mkutano huo, Trump alisema kwamba ni neema ya mwenyezi Mungu ilimwepushia kifo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *