Rais Donald Trump ametangaza kuongezwa marudufu kiwango cha ushuru unaotozwa vyuma vinavyoagizwa kutoka mataifa ya kigeni, kutoka asili mia 25 hadi asili mia 50 kuanzia siku ya jumatano juma lijalo.
Akiongea wakati wa mkutano mmoja wa hadhara huko Pittsburgh, Trump alisema madhumini ya hatua hiyo ni kufufua seka ya vyuma nchini humo na kupunguza kiwango cha vyuma vinavyoagizwa kutoka mataifa ya kigeni hasa kutoka China.
Kiongozi huyo alidokeza pendekezo la kutenga dola bilioni 14 katika juhudi za kuongeza utengezaji wa vyuma nchini humo kupitia ushirikiano na kampuni ya vyuma ya Japan ya Nippon.
Hata hivyio aliongeza kuwa mazungumuzo kuhusiana na mpango huo bado yanaendelea.
Trump pia aliahidi kwamba hakuna mfanyikazi atakayepoteza ajira katika sekta ya vyuma nchini humo kutokana na mpango huo.Hayo yanajiri huku sera za kiuchumi za rais Trump zikiendelea kukabiliwa na upinzani mkali.
Amerika bado inaendelea kuagiza kiwango kikubwa cha vyuma kutoka nje,huku China ikiendelea kuongoza katika utengezaji wa vyuma kote duniani.