Timu za Afrika zilirushwa makundi magumu katika droo ya fainali za klabu Bingwa Duniani mwaka ujao iliyoandaliwa jana usiku mjini Miami Marekani.
Mabingwa wa Afrika Ally Ahly wamejumuishwa kundi A pamoja na Palmeiras ya Brazil,FC Porto ya Ureno na Inter Miami, huku Ahly wakifungua kipute hicho Juni 15 mwakani dhidi ya wenyeji Inter Miami.
Kundi B linasheheni Paris St Germain ya Ufaransa,Atletico Madrid kutoka Uhispania,Botafogo ya Brazil na wenyeji Seattle Sounders.
Bayern Munich ya Ujerumani,Auckland City kutoka Newzealand ,Boca Juniors ya Argentina na Benfica kutoka Ureno zimejumuishwa kundi C ,wakati kundi D likiwa na waakilishi wengine wa Afrika Esperance kutoka Tunisia,Flamingo ya Brazil,Chelsea kutoka Uingereza na Club Leon ya Mexico.
River Plate ya Argentina,Urawa Red Diamonds ya Japan,CF Monterrey ya Mexico na Inter Milan ya Italia zimo kundi E, nao Mamelodi Sundowns kutoka Afrika Kusini wakirushwa kilindini kundini F pamoja na Borusia Dortmund ya Ujerumani,Fluminense ya Brazil na Ulsan Hyundai ya Korea Kusini.
Wydad Casablanca ya Morocco imejumuishwa na manyangumi Manchester City,Juventus na Al Ain ya Milki za Kiarabu, huku mabingwa wa Ulaya Real Madrid wakiunda kundi la mwisho la H pamoja na Al Hilal,Pachuca na Red Bull Salzburg.
Fainali ya kindumbwendumbwe hicho itasakatwa Julai 13 huku Rais wa FIFA Giannni Infantinho akikabindhi mabingwa kombe kwa mara ya kwanza.