Timu ya Kenya ya mbio za nyika Afrika kuondoka kwenda Tunisia

Dismas Otuke
1 Min Read

Wanariadha 30 watakaoiwakilisha Kenya katika malaka ya mwaka huu ya mashindano ya mbio za nyika barani Afrika wameondoka nchini Alhamisi kuelekea mjini Hammamet,Tunisia kwa mashindano hayo yatakayoandaliwa tarehe 25 mwezi huu.

Timu hiyo itaongozwa na John Wachira, itaondoka saa tano kasorobo usiku wa Alhamisi kwa kutumia ndege ya Emirates EK 722 .

Washiriki wa mbio za chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 ni pamoja na Judy Kemunto,Titus Kiprotich,Lucy Nduta,Gideon Kipngetich,Sharon Chepkemoi,Clinton Kimutai,Judy Chepkoech,Simon Maywa,Marion Jepngetich,Joseph Njoroge,Cynthia Chepkurui na Joash Kiprotich.

Timu kilomita 10 watu wazima inawajumuisha Cintia Chepngeno,Naibei Kiplimo,Sandrafelis Chebet,Vincent Langat,Virginia Nyambura,Fredrick Domongole,Glady’s Kwamboka,Robert Kiprop,Caren Chebet,brian Kiptoo,Beatrice Begi na Vincent Kimaiyo.

Waakilishi wa Kenya katika mbio za mseto kupokezana kijiti ni Mirriam Cherop,Evaline Chepkoech,,Winfred Mbithe,Edwin Kiprono,Victor Mutai na Newton Cheruiyot.

Share This Article