Ujumbe wa Kenya unaojumuisha wachezaji na makocha 187 umepokea bendera ya taifa siku ya Jumatatu tayari kushiriki makala ya mwaka huu ya Michezo ya Jumuiya ya Madola, iliyoratibiwa kuandaliwa mjini Glascow Scotland kati ya Julai 23 na tarehe 2 mwezi ujao.
Katibu katika wizara ya Michezo Elijah Mwangi, ameongoza hafla hiyo ya kukabidhi bendera ya taifa katika uwanja wa Kasarani siku ya Jumatatu.
Hafla hiyo aidha,iliongozwa na kamati ya Olimpiki nchini NOC-K ikiongozwa na Naibu Rais wa kwanza Barnaba Korir.
Katibu Mwangi alikariri msimamo wa serikali wa kuinga mkono timu hiyo kwa hali na mali kuhakikisha inasajili matokeo bora.

Kenya ilimaliza ya 13 katika makala ya mwaka 2022 mjini Birmingham,Uingereza kwa medali 21,dhahabu 5 fedha 6 na shaba 10.