Gavana wa jimbo la Nairobi Johnson Sakaja, amepuuzilia mbali uvumi kuwa ada kuegesha magari imeongezwa ,akiwahakikishia wenye magari kuwa ada itasalia ilivyokuwa awali.
Sakaja amewataka wenye magari kuchukulia taarifa hizo kuwa porojo.
Ameongeza kuwa ada ya maegesho ya magari itasalia shilingi 300 kwa siku au shilingi 5,000 kwa mwezi mmoja kwa magari madogo.
Magari aina ya Vans na Pick -Ups yatatozwa shilingi 500 kwa siku huku malori,na mabasi madogo yakitozwa ada ya shilingi 1,000 kwa siku ama shilingi 12,500 kwa mwezi.
Hata hivyo, wenye magari hawatatozwa ada ya kuegesha magari siku za Jumamosi na Jumapili.