Timu ya Kenya iliyotwaa ubingwa wa mbio za barabara duniani kurejea Jumatatu usiku

Dismas Otuke
1 Min Read

Kikosi cha Kenya kilichonyakua  ubingwa wa dunia katika mbio za barabarani mjini Riga ,Latvia kitarejea nchini Jumatatu usiku.

Timu hiyo ilinyakua medali 5 za dhahabu,3 za fedha na 4 shaba ,wakitamalaki mbio za nusu marathon walizotwaa medali zote tatu kwa wanume na pia wanawake.

Peres Jepchir na Sebastien Sawe walishinda dhahabu za nusu marathon huku Beatrice Chebet akitwaa  dhahabu ya kilomita 5 .

Dhahabu nyingine mbili zilinyakuliwa na timu za nusu marathoni kwa jumla huku Daniel Simiu na Margaret Chelimo, wakinyakua fedha katika nusu marathoni na Lillian Kasait katika kilomita tano.

Medali nne za shaba zilipatikana kupitia kwa Catherine Relin na Samwel Mailu katika nusu marathoni,Nicholas Kipkorir katika kilomita tano na Faith Kipyegon katika mbio za maili moja.

Share This Article