Mvua kubwa inatarajiwa kushuhudiwa katika kaunti ya Nairobi na virunga vyake kati ya leo Ijumaa na Jumamosi.
Idara ya utabiri wa hali ya hewa imewatahadhari raia kuwa waangalifu kutoka na uwezekano wa kuwepo kwa mafuriko hususan kwenye maeneo yaliyo tambarare.
Haya yanajiri takriban juma moja baada ya mvua kubwa kusababisha mafuriko yaliyowasomba na kuwaua watu 49, katika maeneo kadhaa ya kaunti ya Nairobi.