Tanzania yapiga marufuku ndege za abiria za shirika la KQ kati ya Nairobi na Dar es salaam

Tom Mathinji
1 Min Read

Serikali ya Tanzania imepiga marufuku safari za ndege za abiria za shirika la Airways (KQ), kati ya Nairobi na Dar es Salaam.

Halmashauri ya safari za ndege ya Tanzania (TCAA), ilisema agizo hilo litatekelezwa kuanzia tarehe 22 mwezi Januari mwaka 2024.

Kupitia kwa taarifa, Mkurugenzi mkuu wa halmashauri ya TCAA Hamza Johari, alisema marufuku hayo yamesababishwa na hatua ya Kenya ya kukataa ombi la Tanzania la kuwepo kwa safari za ndege za mizigo za shirika la ndege la Tanzania.

“Hatua hii inatokana na Kenya kukataa ombi la Tanzania la kuwepo kwa safari za ndege za migizo za Shirika la ndege la Tanzania kati ya Nairobi na mataifa mengine, kinyume na mkataba wa maelewano kati ya kuhusu safari za angani kati ya Kenya na Tanzania iliyotiwa Saini tarehe 24 mwezi Novemba mwaka 2016 Jijini Nairobi,” alidokeza Johari.

Aidha Johari aliongeza kuwa “Kufuatia hatua hiyo, hakutakuwa na safari za ndege za abiria kati ya Nairobi na Dar kuanzia tarehe 22 mwezi  Januari 2024,”.

TAGGED:
Share This Article