Tanzania imefungua tena mnada wa madini ya vito ulio katika wadi ya Mirerani eneo la Manyara, baada ya kupiga marufuku uuzaji madini kwa mnada miaka saba iliyopita.
Waziri wa Madini Anthony Mavunde akizungumza Jumamosi iliyopita alipofungua mnda huo, alisema hatua hiyo inalenga kuwainua kiuchumi wakazi wa eneo hilo wanaotegemea madini hayo.
Mnada huo uliwashirikisha wachuuzi 59 wanaouza vito kwa kiwango kikubwa na wengine 120 wanaouza rejareja.
Hatua hiyo inalenga kuzuia uuzaji na uagizaji wa madini hayo kimagendo.
Waziri Mavunde awali, mwezi Oktoba mwaka huu, alitangaza kuwa mnada huo utakuwa ukiendeshwa mara nne kwa mwaka katika miji ya Dar e Salaam, Arusha na Zanzibar.