Tanzania: Mabalozi watakiwa kutafuta fursa

Francis Ngala
2 Min Read
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka mabalozi kufuatilia utekelezaji wa mikataba na hati za makubaliano zinazotokana na ziara za viongozi ndani na nje ya nchi.

Akiongea hii leo katika hafla ya kuwaapisha mabalozi wateule, Rais Samia amewataka mabalozi kuwa na mikakati katika utekelezaji wa majukumu yao na sio kuendeshwa na matukio.

“Tanzania hatuwezi kufanya kazi peke yetu, tunahitaji wenzetu na sisi tunahitajika kwa wenzetu, na ndio maana tunakwenda katika nchi hizo kuwakilisha taifa letu kwao,” alisema Rais Samia Suluhu wakati wa kuwaapisha mabalozi wateule Ikulu, Chamwino.

Aidha amewataka mabalozi kuibua masuala ya ushirikiano katika vituo vyao vya kazi na kutafuta fursa mbalimbali ikiwemo katika sekta ya uwekezaji, utalii pamoja na mahitaji ya ng’ambo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka: Picha – Ikulu mawasiliano

Vile vile amewaonya mabalozi wazembe kazini na kuwataka kuwajibikia masuala ya taifa hilo kwa kuhakikisha wanakuwa kipaumbele katika kuitangaza Tanzania katika nchi husika.

“Nilazima tukubali sio kila balozi zina fursa za kupata mitaji, mikopo ya riba nafuu, biashara na uwekezaji, kuna balozi nyingine wajibu wao mkubwa ni kutetea msimamo wa nchi yetu na kuikingia kifua Tanzania,” aliongeza Suluhu.

Soma zaidi: Hampati ng’oo! Rais Ruto asisitiza hakuna serikali ya ‘nusu mkate’

Share This Article
Follow:
I am Versatile Multimedia Journalist with years of experience in Digital platforms, Live TV and Radio. In another world am a News Anchor and Reporter.
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *