Tanzania haitakubali kuelekezwa na mataifa ya kigeni, asema Suluhu

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kamwe hatakubali kushurutishwa na mataifa ya kigeni kuhusu kile anachohitaji kufanya.

Akihutubu katika uwanja wa kijeshi mjini Dodoma punde baada ya kuapishwa, Suluhu amekiri kuwapo kwa dosari kadhaa ila uchaguzi uliendeshwa vyema.

Ameahidi kufanya marekebisho siku zijazo ila akakariri kuwa kamwe hatachukua maelekezo kutoka kwa waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi mkuu uliopita.

Rais Suluhu alipata asilimia 98 ya kura zilizopigwa aliposhindana na wapinzani wengine 16.

Wachambuzi wa mambo wanasema 16 hao walikuwa wapinzani hafifu waliotumiwa na utawala wa nchi hiyo kuhalalisha uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 baada ya wapinzani wakuu kuzuiwa kushiriki.

Website |  + posts
Share This Article