Tamasha la Roast and Rhyme nchini Uganda linarejelewa Jumapili hii Novemba 3, 2024, katika eneo la ufuoni mwa ziwa Viktoria la Jahazi Pier, Munyonyo jijini Kampala.
Waandalizi wa awamu hiyo ya 22 ya Roast and Rhyme wanahimiza wanaotaka kuhudhuria kufika mapema kuanzia saa tano asubuhi ili kufurahia mandhari, muziki na chakula hasa nyama choma.
Iryn Namubiru, amepangiwa kuwa mtumbuizaji mkuu wa tamasha hilo pamoja na wasanii wengine kama Maro na ZuliTums.
Watakaohudhuria wanahimizwa kubeba vifaa vyao vya kuchomea nyama.
Tamasha la Roast and Rhyme lilianzishwa mwaka 2016 nchini Uganda na kadri miaka inavyosonga limekuwa likivutia mashabiki hata wa nchi za nje.
Tiketi za mapema zinauzwa shilingi elfu 70, za Uganda sawa na shilingi 2500 za Kenya huku za kwenye lango siku hiyo zikiuzwa elfu 100 pesa za Uganda sawa na shilingi 3500 za Kenya.