Takriban watu 500 wauawa Lebanon katika mashambulizi ya Israel

Dismas Otuke
1 Min Read

Angaa watu 500 wameuawa katika mashambulizi makali ya angani yaliyotekelezwa mapame leo na wanajeshi wa Israel wakiwalenga wanamgambo wa Hezbollah mjini Lebanon.

Shambulizi hilo limetajwa na  wizara ya afya kuwa baya zaidi kwa miongo miwili iliyopita.

Maelfu ya familia zimetoroka makwao huku majeshi ya Israel yakisema yalilenga maeneo 1,300 ya kundi la Hezbollah, ambalo limekuwa likijiandaa kwa vita tangu mwaka 2006.

Hezbollah,pia walirusha roketi zaidi ya 200 kaskazini mwa Israel na kuwajeruhi watu wawili kulingana na matabibu.

Mataifa yenye uwezo mkubwa duniani yamekuwa yakiomba pande hizo mbili kusitisha mapigano ili yasisababishe vita.

Kwa mjibu wa Wizara ya afya watoto 35 na wanawake 58 ni miongoni mwa walioangamia kwenye shambulizi hilo, huku watu wengine 1,645 wakijeruhiwa.

Share This Article