Taasisi za AU zinapaswa kufanyiwa marekebisho, asema Rais Ruto

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais Ruto ashauriana na Rais wa bunge la Afrika Zephaniah Charumbira.

Rais William Ruto ameelezea haja ya kufanyiwa marekebisho taasisi zilizoko katika Umoja wa Afrika, ili kuuwezesha kuboresha huduma kwa wananchama wake 55.

Kiongozi wa taifa alisema tume ya Umoja wa Afrika inapaswa kupewa mamlaka zaidi ya kutoa maamuzi, huku bunge la Afrika lipewe mamlaka zaidi ya uangalizi wa tume hiyo.

Rais aliyasema hayo alipokutana na Rais wa bunge la Afrika Zephaniah Charumbira, pamoja na maafisa wengine kujadili mustakabal wa Muungano wa Afrika.

Mkutano huo ulisisitiza kujitolea kwa Kenya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kuzipa nguvu taasisi za bara Afrika, ili kukabiliana na changamoto zinazoshuhudiwa katika kanda hii, zikiwemo za kiusalama na uongozi.

Mkutano huo uliandaliwa katika ikulu ya Nairobi siku ya Jumanne.

TAGGED:
Share This Article