Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, alifanya mkutano na ujumbe viongozi wa kimataifa katika makazi yake mtaani Kareni kaunti ya Nairobi siku ya Ijumaa.
Kalonzo amethibitisha kukutana na maafisa kadhaa wa jamii ya kimataifa kutoka Canada na Marekani,ingawa hakufichua kiini cha majadiliano yao.
Yamkini ujumbe huo ulimwekea shinikizo Kalonzo na upinzani kusitisha maandamano dhidi ya serikali.
Maandamano ya siku tatu yaliyoitishwa na upinzani kuanzia jumatano hadi Ijumaa wiki hii yalisababisha uharibu mkubwa na maafa .