Susan Ejore afuzu kwa fainali ya mita 1500 mashindano ya Dunia

Dismas Otuke
1 Min Read

Susan Ejore amefuzu kwa fainali ya mita 1,500 katika mashindano ya dunia ya ukumbini yaliyoanza leo mjini Nanjing, Uchina./strong>

Ejore amefuzu baada ya kumaliza wa tatu katika mchujo wa kwanza kwa kutumia dakika 4 sekunde 12.41.

Fainali ya mbio hizo itaandaliwa Jumapili hii.

Lillian Odira amefuzu kwa nusu fainali ya mita 800 baada ya kumaliza wa pili katika mchujo wa kwanza kwa kutumia dakika 2 sekunde 4.46.

Nusu fainali ya mbio hizo itaandaliwa kesho.

Website |  + posts
Share This Article