Sun King yazindua mtambo wa Powerhub inverter wa kilowati 30

Mtambo huo maarufu kama Powerhub inverter unauwezo wa kuhifadhi kawi ya miale ya jua kati ya kilowati 2 hadi 30 kulingana na idadi ya viwambo .

Dismas Otuke
1 Min Read

Kampuni ya Sun King imezindua mtambo mkubwa wa kuzalisha nishani ya jua wa kilowati 30 nchini Kenya katika juhudio za kuongeza matumizi ya kawi safi ya miale ya jua.

Mtambo huo maarufu kama Powerhub inverter unauwezo wa kuhifadhi kawi ya miale ya jua kati ya kilowati 2 hadi 30 kulingana na idadi ya viwambo .

Kulingana na sun King Mtambo huo unaogharimu shilingi laki tatu unusu au malipo ya polepole unaweza kutumika vyema kwa kutega nishati ya jua inayoweza kutimika kwa mashine za kusukuma maji,Microwaves,mashine ya kufua pamoja na kuendesha mitambo ya hospitalini.

Idadi zabaini kuwa mtu mmoja kati watano anatumia nishati itokanayo na miale ya jua wakati Sun King ikilenga kuongeza idadi hiyo hadi mmoja kati ya watatu.

 

Share This Article