Sukyan Omar Hassan ateuliwa kaimu Kadhi Mkuu wa Kenya

Tom Mathinji
1 Min Read
Sukyan Omar Hassan achaguliwa kaimu Kadhi Mkuu wa Kenya.

Sukyan Omar Hassan amechaguliwa Kaimu Kadhi Mkuu wa Kenya kuanzia Agosti 6, 2025.

Uteuzi wake unafuatia kifo cha ghafla cha Kadhi Mkuu Sheikh Athman Abdul-Halim Julai 10, 2025.

Hassan kwa sasa ni Kadhi Mkuu Mwandamizi.

Kupitia kwa taarifa iliyotolewa na Msajili Mkuu wa Idara ya Mahakama Winfridah Mokaya, Tume ya Huduma za Mahakama (JSC), ilisema hatua hiyo iliafikiwa wakati wa mkutano ulioandaliwa Julai 14, 2025, kuambatana na sehmu ya 170 ya Katiba, ibara ya 2 ya sheria za Mahakama za Kadhi.

“Tume ya Huduma za Mahakama, iliandaa mkutano Julai 14, 2025 kuamabatana na sehemu ya 170 ya Katiba, ibara ya 2 ya Mahakama za Kadhi, na kuidhinisha uteuzi wa Kadhi aliye wadhifani kuchukua nafasi ya Kadhi Mkuu,” ilisema taarifa hiyo.

“Wadhifa wa Kadhi Mkuu ulisalia wazi kufuatia kifo cha Athman Abdul-Halim Julai 10, 2025. Wakati huo huo, Sheik Sukyan Omar Hassan, Kadhi Mkuu Mwandamizi, ameteuliwa kuwa kaimu Kadhi Mkuu kuanzia Agosti 6, 2025.”

Kulingana na tume hiyo, Hassan atashikilia wadhifa huo kwa kipindi cha muda wa miezi mitatu au hadi wadhi huo utajazwa kikamilifu. Atakuwa Kadhi wa 12 wa wadhifa wa Kadhi Mkuu.

Website |  + posts
Share This Article