Sudan Kusini imeshauriwa kuahirisha uchaguzi wake mkuu uliopangwa kuandaliwa Disemba mwaka huu kwa kukosa mipango madhubuti ya kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki.
Kundi la ushauri linalowajumuisha watu wa Sudan na makundi ya kijamii ya Kenya, limeitaka Sudan Kusini kusongeza mbele tarehe ya uchaguzi mkuu, hadi sera mwafaka za kuleta uwazi na uwajibikaji zibuniwe.
Waakilishi wa mashirika 22 yaliyokutana Nairobi mapema mwezi huu,walisema nchi hiyo haiko tayari kwa uchaguzi mkuu.
Sudan Kusini imekosa kubuni sera zitakazoongoza uchaguzi, wakati ambapo makundi kadhaa yamesi kuachwa nje ya serikali ya Rais Salva Kiiri iliyobunia mwaka 2008.