Kocha wa Barcelona Xavi Hernandez amethibitisha kuwa winga Ousmane Dembele raia wa Ufaransa anataka kujiunga na klabu ya Paris Saint Germain katika dirisha hili la majira ya joto.
Akizungumza hayo jana Jumanne baada ya ushindi wa bao moja kwa nunge dhidi ya AC Milan, Xavi alisema hatua ya Dembele inamsikitisha mno na hakuna la ziada ambalo miamba hao wa Uhispania wanaweza kulifanya kwa sasa.
“Dembele alituambia anataka kuondoka,” alisema Xavi.
“Ninakerwa sana. Dembele alipokea dau la maombi ya kujiunga na PSG na hatuwezi tukafanya lolote. Hatuwezi tukashindanisha kitita chetu na PSG, hatuna uwezo wa kushindana na PSG. Hivi ndivyo hali ya soko ilivyo, na wachezaji ambao hawataki kuendelea na Barcelona basi itabidi waondoke, lakini pia kuondoka kwa Dembele kunatudhoofisha,” Xavi aliendelea.
🎙️ Xavi: “Dembélé came and told me he wanted to leave. He has an offer from PSG that we cannot match.” pic.twitter.com/VHfeB065mj
— FC Barcelona (@FCBarcelona) August 2, 2023
MKONDO WA BARCELONA NI UPI?
Kuondoka kwa Ousmane Dembele ni wazi kwamba kutawaacha wenye uhitaji mkubwa wa winga aliye na uzoefu hata ingawa klabu hiyo ya Uhispania inaingia msimu ujao ikiwa na vijana tofauti waliojaaliwa vipaji.
Robert Lewandowski ataongoza kikosi cha kwanza cha wachezaji 11 wa klabu hiyo huku kinda Ansu Fati ambaye amejithibitisha katika mchuano wa AC Milan akitajwa kuwa mwenyeji katika kikosi hicho pamoja na Lamine Yamal wa Akademia ya La Masia.
SOMA ZAIDI: Gianluigi Buffon aamua kutundika daluga