Spika Wetang’ula kutoa msaada wa tarakilishi kwa taasisi ya mapadri

Marion Bosire
1 Min Read

Spika wa bunge la taifa Moses Wetang’ula ameahidi kutoa msaada wa tarakilishi 100 kwa taasisi ya kutoa mafunzo kwa wanaotaka kuwa mapadri wa kanisa Katoliki ya Mtakatifu Augustine.

Wetang’ula alizuru taasisi hiyo iliyoko katika eneo la Mabanga, wadi ya Nalondo Magharibi, eneo bunge la Kabuchai, kaunti ya Bungoma ambako alishauriana na msimamizi wake Padri Protus Osyanju.

Osyanju alimfahamisha kuhusu changamoto kadhaa zinazokumba taasisi hiyo kama vile ugumu wa wanafunzi kutoka Tanzania kupata vibali vya kuingia nchini Kenya.

Aliahidi kusaidia wanafunzi hao pamoja na wengine kutoka mataifa ya Afrika Mashariki kuingia nchini kwa urahisi na kusaidia katika ujenzi wa bweni la kisasa.

Kiongozi huyo aliwasihi wanafunzi wa taasisi hiyo wanaosomea upadri kujitolea kwa mwito wao.

Aliwataka pia waendeleze safari hiyo ikitizamiwa jukumu lao muhimu la kuhimiza maadili mema katika jamii.

Hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Wetang’ula kuzuru taasisi hiyo.

Website |  + posts
Share This Article