Spika Wetangula achapisha uidhinishaji wa Kindiki

Dismas Otuke
0 Min Read

Spika wa Bunge la kitaifa Moses Wetang’ula  amechapisha kwenye Gazeti rasmi la serikali uidhinishaji wa Professor Kithure Kindiki, kuwa Naibu Rais Mpya kufuatia kung’atuliwa kwa Rigathi Gachagua.

Hii inafuatia  Wabunge 236 kupiga kura ya kuunga mkono hatua ta Rais William Ruto, kumteua Kindiki, kuwa Naibu wake mapema Ijumaa .

Spika  Wetang’ula  baada ya kuchapisha kwenye gazeti uidhinishaji huo wa Kindiki unapisha njia kwa uapisho wake Kindiki.

Share This Article