Spika wa Bunge la kitaifa Moses Wetang’ula, ametaka kuharakisha kwa kubuniwa kwa tume huru ya mipaka na uchaguzi nchini IEBC, huku bunge likijipanga kurejelea vikao wiki hii.
Wetang’ula amasema haya Jumapili alipohudhuria ibada ya misa katika kanisa la Katoliki la Chebukwa kaunti ya Bungoma.
Spika amesema kuwa ipo haja ya kuharakishwa kwa mchakato wa kuteua Makamishna wa IEBC, kusaidia kurejelewa kwa shughuli nyingi za tume hiyo zilizokwama kutokana na kukosa kwa Makamishna.
“Hatuwezisubiri zaidi kubuniwa kwa tume ya IEBC,kuna chaguzi nyingi ndogo za mabunge ya kaunti ,na bunge la kitaifa ambazo hazijaandaliwa.Ninahimiza wale wanaoweka vikwazo waviondoe na kuruhusu nchi iendelee mbele.”akasema Spika Wetangula
Wetang’ula amemtaka pia Jaji Mkuu na afisi yake kuharakisha kesi zote zilizowasilishwa dhidi ya IEBC, ili kuruhusu shughuli za kawaida kuendelea.
Bunge la kitaifa linatazamiwa kurejea vikao vyake Jumanne Septemba 17.