Somalia kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC

Dismas Otuke
1 Min Read

Somalia inatarajiwa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC kabla ya mwishoni mwa mwezi Novemba, 2023. 

Hii ni kulingana na Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo Dkt. Peter Mathuki.

EAC inatarajiwa kuandaa kongamano la Marais wa jumuiya hiyo kati ya Novemba 23 na 24.

Ombi la Somalia kutaka kuwa mwanachama wa EAC linatarajiwa kuidhinishwa wakati wa kongamano hilo.

Mathuki amesistiza kuwa jumuiya hiyo inaangazia pakubwa maslahi ya wanachama na kukariri mchango muhimu wa mashirika ya kibinafsi katika kuleta mtagusano wa kikanda.

Share This Article