Sogora wa Tennis Rafael Nadal astaafu akiwa na umri wa miaka 38

Dismas Otuke
1 Min Read

Gwiji wa tennis Rafael Nadal wa Uhispania ametangaza kustaafu akiwa na umri wa miaka 38 baada ya kushinda mataji 22 ya Grand Slam .

Nadal,amecheza kwa miaka 23 akitwaa mataji 14 ya French Open, lakini ametatizwa na majeraha kwa muda mrefu.

Pia Mspanyola huyo alishinda mataji mawili ya Australia Open,mawili ya Wimbledon Open na manne ya US Open.

Nadal pia alinyakua dhahabu ya Olimpiki mwaka 2008 kwa mchezaji mmoja na nyingine wachezaji wawili wawili.

Share This Article