SOFAPAKA wameweka hai matumaini ya kusalia ligi kuu ya FKFPL msimu ujao, baada ya kuwazabua Naivas FC bao moja bila jibu katika duru ya kwanza ya mchujo wa kushiriki Ligi.
Jacob Onyango alipachika goli la pekee kwa wageni SOFAPAKA almaarufu Batoto Ba Mungu, kunako dakika ya 89 katika uwanja wa Police Sacco.
Mchuano wa marudio utapigwa katika uchanjaa wa Dandora Julai 14, huku mshindi wa jumla akifuzu kushiriki Ligi Kuu msimu ujao.
Naivas ilimaliz ya tatu katika ligi kuu ya taifa pana NSL, wakati Sofapaka ikimaliza ya 16 kwenye Ligi Kuu ya FKF.
Sofapaka ambao ni mabingwa wa Ligi kuu mwaka 2009, wanawania kusalia ligini tangu walipopandshwa ngazi huku Naivas wakiwania kushiriki Ligi kuu kwa mara ya kwanza.