Mwamuzi wa Slovenia Slavko Vinčić,ameteuliwa kuwa msimamizi wa fainali ya Kombe la Dunia kati ya Uhispania na Mabingwa watetezi Argentina Jumapili hii katika uwanja wa Metlife mjini New York.
Refarii huyo atasaidiwa na Tomaž Klančnik na Andraž Kovačič,wote kutoka Slovenia, huku Adham Makhadmeh wa Jordan akiwa afisaa wa nne.
Itakuwa mechi ya nne kwa mwamuzi huyo kusimamia katika kipute cha mwaka huu baada ya kuwa Pilato wa mchuano wa kundi C, kati ya Brazil na Morocco,ule kati ya Jordan na Algeria na mechi ya awamu ya 32, baina ya Mexico na Ecuador.
Aidha,Vinčić alikuwa refarii wa kwanza kutoa kadi nyekundu kwa beki wa Ecuador Piero Hincapié, baada ya kumwongelesha mchezaji wa Mexicor akiwa amefumba mdomo.
Argentina watalenga kutwaa kombe la nne hali kadhalika kuhifadhi taji hiyo wakati Uhispania wakiwinda Kombe la pili.