Mr. Gave afariki

Chanzo halisi cha kifo chake pamoja na mazingira yaliyozunguka kifo hicho bado havijajulikana.

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki wa Kongo DRC, Mr Gave, anayejulikana sana kama Forca Le Mwami, alifariki usiku wa tarehe 16 Julai 2026.

Mzaliwa huyo wa eneo la Uvira, mkoa wa Kivu Kusini, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, alifariki ghafla, kifo chake kikiacha wahusika wa ulimwengu wa sanaa na utamaduni wa eneo hilo katika mshtuko mkubwa na maombolezo.

Baada ya kufariki, mwili wake ulihamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Uvira kwa ajili ya kuhifadhiwa.

Hadi kufikia tarehe 17 Julai 2026, chanzo halisi cha kifo chake pamoja na mazingira yaliyozunguka kifo hicho bado hayajajulikana.

Mashabiki pamoja na mamlaka za eneo hilo wanaendelea kusubiri taarifa rasmi kutoka kwa familia yake na wahudumu wa afya.

Mr Gave alikuwa mmoja wa wasanii waliotambulika sana katika medani ya muziki wa Uvira, akiheshimika kwa kipaji chake na mchango wake mkubwa katika kuendeleza shughuli za sanaa na burudani mjini humo.

Share This Article