Sing’Oei: Maafisa wa Kenya wamemtembelea Nduta gerezani

Tom Mathinji
2 Min Read
Katibu katika wizara ya Mambo ya Nje Korir Sing'Oei.

Katibu katika wizara ya Mambo ya Nje  Korir Sing’Oei, amesema kuwa maafisa wa kibalozi wa Kenya kutoka Bankok wamepata hati za kusafiri hadi Vietnam na kumtembelea Margaret Nduta anayezuiliwa katika gereza la Hoi Chin Mihn.

Kupitia ukurasa wa X, Sing’Oei alidokeza kuwa ingawqa Nduta ametatizika kimawazo na swala hilo, hata hivyo anahudumiwa vyema katika gerezani hilo.

“Tuna fahari kuwafahamisha kuwa kundi letu kutoka Bankok, likifanikiwa kupata vyeti vya kusafiri na kuelekea katika gereza la Hoi Chin Mihn ambako Margaret Nduta anazuiliwa,” ilisema taarifa ya Katibu huyo.

Katibu huyo alidokeza kuwa Nduta hakuwakilishwa na wakili katika kesi iliyomkabili ya ulanguzi wa mihadarati, lakini serikali ya Kenya imewasilisha rufaa dhidi ya kesi hiyo kwa niaba ya nduta.

“Licha ya kwamba Nduta hakuwakilishwa na wakili katika kesi hiyo, rufaa iliyowasilishwa na Kenya kwa niaba yake itasikizwa hivi karibuni,” aliongeza Katibu huyo.

Aidha, alisema serikali ya Kenya inaendelea kushauriana na serikali ya Vietnam kuhusu njia mbadala ya kutatua swala hilo alilolitaja kuwa ngumu.

Wakati huo huo, aliwatahadharisha wakenya dhidi ya kujihusisha katika ulanguzi wa mihadarati.

Nduta alitiwa mbaroni mwaka 2023 baada ya kuwasili kwa ndege nchini Vietnam akiwa na kilo mbili za dawa ya kulevya aina ya Cocaine. Hatahivyo familia inashikilia kwamba alihadaiwa.

Website |  + posts
Share This Article