Klabu ya Simba ndio mabingwa wa mwaka 2026, wa kombe la Muungano, baada ya kuwalemea watani wa jadi Yanga bao moja kwa bila.
Fainali hiyo ya Jumatano usiku katika uwanja wa Amaan, kisiwani Zanzibar, ilikuwa ya kuadhimisha miaka 60, ya Muungano wa kisiwa cha Zanzibar na Tanzania bara.
Bao pekee na la ushindi kwa Wekundu wa Msimbazi, lilipachikwa kimiani na Selemani Mwalimu, kupitia tuta la penati.
Fainali hiyo pia ilikuwa vita kati ya Wakenya Mohammed Bajaber wa Simba, na kiungo Duke Abuka wa Yanga, waliojumuishwa
katika kipindi pili.
Simba wamefanya gwaride Alhamisi katika barabara za Dar es Salaam, kusherehekea ushindi wa kombe hiloar es Salaam: