Limbukeni Cape Verde kujitosa baharini dhidi ya Uhispania Jumatatu

Ubelgiji na Misri watakutana kwa mara ya kwanza katika historia katika mechi ya kundi G nchini Marekani.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2010 ambao wanashikilia nafasi ya pili duniani Uhispania, watashuka uwanjani Mercedes Benz mjini Atlanta Marekani Jumatatu kuanzia saa moja usiku kwa mechi ya ufunguzi ya kundi H dhidi ya Cape Verde wanaoshiriki kwa mara ya kwanza.

Itakuwa mara ya kwanza kwa Cape Verde maarufu kama Blue Sharks, kumenyana na Uhispania katika Kombe la Dunia.

Ubelgiji na Misri watakutana kwa mara ya kwanza katika historia katika mechi ya kundi G nchini Marekani.

Ubelgiji wanaoshikilia nafasi ya 9 duniani watachuana na Misri iliyo ya 29, huku Mafarao wakiwinda ushindi wa kwanza katika historia ya Kombe la Dunia.

Share This Article