Simba na Yanga watinga makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika

Dismas Otuke
1 Min Read

Klabu za Tanzania ,Simba na Yanga zimetinga hatua ya makundi ya kuwania kombe la Ligi ya Mabingwa barani Afrika msimu wa mwaka 2023/2024.

Simba maaraufu kama wekundu wa Msimbazi au Mnyama walitinga hatua ya makundi kwa mara ya sita  siku ya Jumapili kwa magoli ya ugenini, baada ya mechi yao kumalizikia sare ya  ya 1-1 uwanjani  Azam  Complex, dhidi ya Power Dynamos kutoka Zimbabwe.

Duru ya kwanza ilikuwa imeishia sare ya 2-2 mjini Harare.

Young Africans almaarufu Yanga ukipenda vijana wa Jangwani waliandikisha ushindi wa jumla wa magoli matatu kwa bila dhidi ya Almerreikh ya Sudan na kuingia hatua ya makundi kwa mara ya kwanza baada ya subira ya miaka 25.

Mchuano wa marudio wa raundi hiyo ya mwondoano ulisakatwa Jumamosi ugani Chamazi Complex ,Yanga wakidedea moja kwa bili kuongezea kwa ushindi wa mabao mawili kwa nunge katika duru ya kwanza.

Simba na Yanga ndio waakilishi pekee wa ukanda wa CECAFA katika hatua ya makundi ya ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

Katika kombe la shirikisho la soka Afrika ,ukanda wa CECAFA utakosa mwakilishi kufuatia kuenguliwa kwa timu ya Kampala ya Uganda kwenye mchujo wa pili.

Share This Article