Timu ya Kenya ya raga kwa wanawake saba upande maarufu Lionnesses, itachuana na Colombia leo jioni katika semi fainali ya kombe la Challenger mjini Cape Town Afrika Kusini.
Kenya ilifungua msururu wa pili kwa kushinda mechi zote za kundi A jana ilipowanyuka Ubelgiji alama 17-5, kabla ya kuibwaga Uganda pointi 10-5.
Nusu fainali ya Kenya na Colombia itang’oa nanga saa kumi na dakika 18 leo alasiri.
Lionesses waliotwaa ubingwa wa msururu wa kwanza wiki jana kwa alama 20 watafuzu kwa raundi ya pili itakayoandaliwa Krakow Poland, huku timu nne bora zikifuzu kwa mchujo wa mwisho utakaondaliwa mjini Los Angeles Marekani.