Kilabu ya Simba imeratibiwa kuchuana na Stellenbosch ya Afrika Kusini kwenye nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Wekundu wa Msimbazi wataanzia nyumbani Dar atrehe 20 mwezi huu, kabla ya kuzuru Afrika Kusini Aprili 27.
Ni mara ya kwanza kwa Simba kutinga semi fainli ya taji hiyo.
RS Barkane watamenyana na Constantine ya Algeria ,wakiianzia Morocco kabla ya marudio kupigwa Algeria.