Siku kuu ya Utamaduni ambayo uadhimishwa hapa nchini tareke 10 mwezi Oktoba, imebadilishwa jina na sasa itakuwa siku ya Mazingira.
Hatua hiyo inalenga kuimarisha utunzaji wa mazingira hapa nchini, katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Siku ya Mazingira itakuwa siku ambayo wakenya wote watashiriki katika shughuli za kuhifadhi mazingira, ikiwa ni pamoja na kupanda na kukuza miti.
Hatua hii inaendana na msukumo wa serikali wa kuharakisha mpango wa miaka 10 wa upandaji miti wa bilioni 15 unaojumuisha urejeshaji wa misitu, ardhioevu na nyanda za malisho.
Mabadiliko hayo yanajumuishwa katika mswada marekebisho ya sheria za bunge, uliotiwa saini leo Jumatano kuwa sheria na Rais William Ruto, katika ikulu ya Nairobi.
Hapo awali siku hii ilijulikana Moi Day, kabla ya kubadilishwa jina kuwa Huduma Day, kisha Utamaduni Day na sasa Mazingira Day.